Psalms 61

Kuomba Ulinzi

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi.

1 aEe Mungu, sikia kilio changu,
usikilize maombi yangu.

2 bKutoka miisho ya dunia ninakuita,
ninaita huku moyo wangu unadhoofika;
uniongoze kwenye mwamba
ule ulio juu kuliko mimi.
3 cKwa kuwa umekuwa kimbilio langu,
ngome imara dhidi ya adui.

4 dNatamani kukaa hemani mwako milele,
na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.
5 eEe Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu,
umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

6 fMwongezee mfalme siku za maisha yake,
miaka yake kwa vizazi vingi.
7 gYeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele;
amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

8 hNdipo daima nitaliimbia sifa jina lako
na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.
Copyright information for SwhNEN